mke kushika mimba
Ili kufahamu vizuri ni siku zipi ni hatari kwa mwanamke kupata mimba, unahitaji kwanza kujifunza jinsi mzunguko wa hedhi (menstrual cycle) unavyofanya kazi.
Kwa wastani, mzunguko wa hedhi huwa ni siku 28.
Mzunguko wa hedhi unaanza kuhesabiwa siku ya kwanza wakati mwanamke anaanza kuona siku zake (kublidi) na tunaiita ni siku ya Kwanza.
1. Idadi ya siku katika mzunguko mmoja (cycle length)
Kwa kawaida idadi ya siku katika mzunguko ambazo huhesabika kama ni mzunguko wa kawaida ni siku 21 hadi 35 (na ni hapo ndipo tunapata wastani wa siku kuwa 28 yaani [(21+35)÷2].
Hivyo mpendwa msomaji wangu usikariri kuwa mzunguko wa kila mwanamke ni siku 28. Wapo wanawake wana mzunguko wa siku 27, wengine 25, wengine 35, wengine 29.
2. Sifa ya pili ni uwiano wa idadi ya siku za mzunguko kati ya mzunguko mmoja na mwingine
Hili nalo ni miongoni mwa changamoto kubwa sana katika suala zima la tendo la ndoa kwani inaweza kuwa vigumu kuzitambua siku hatari kwa mwanamke kubeba ujauzito.
Ili tuhitimishe kwamba mwanamke ana mizunguko ya hedhi iliyo sawa (regular cycles), idadi ya siku za mizunguko ya hedhi haitakiwi itofautiane kwa zaidi ya siku 7.
Mfano, kama mwezi wa kwanza uliona siku zako baada ya siku 28, mwezi wa pili ukaona baada ya siku 30, mwezi wa tatu ukaona baada ya siku 35 na mwezi wa nne ukaona baada ya siku 21, bado mzunguko wako uko kwenye uwiano mzuri (regular cycle) kwa kuwa mzunguko mmoja na mwingine haujatofautiana kwa zaidi ya siku 7.
Hivyo usikariri kwamba siku za mzunguko wa hedhi kwa kila mwanamke ni siku 28, hilo halipo.Hizi siku 28 ni wastani tu.
Wengine wanaona siku zao kila baada ya siku 21, wengine kila baada ya siku 25, wengine 29, wengine 35 na bado tunasema mizunguko yao bado ni mizunguko ya kawaida.
Pia fahamu ya kuwa si lazima idadi ya siku katika mzunguko mmoja ilingane na mzunguko mwingine kwa mwanamke huyo huyo. Mfano usitarajie kuwa kama mwezi wa tatu (march) ameona siku zake baada ya siku 28 na mwezi wa nne (april) pia ataona siku zake baada ya siku 28. Si lazima itokee hivyo lakini pia huwa inaweza kutokea.
Mfano, mwanamke mmoja mzunguko huu anaweza kuona siku zake baada ya siku 28, mzunguko unaofuata baada ya siku 27, mzunguko mwingine baada ya siku 30, mzunguko mwingine baada ya siku 29, mzunguko mwingine baada ya siku 25 na bado yuko kwenye uwiano sawa kwakuwa tofauti si zaidi ya siku 7 kama nilivyoeleza pale juu.
3. Idadi ya siku za kuona siku zake
Usichanganye kati ya siku za hedhi (menstrual period) na mzunguko wa hedhi (menstrual cycle) kwani hivi ni vitu viwili tofauti kabisa.
Siku ya kwanza ya kuona siku zako ndiyo siku tunaanza kuhesabu mzunguko wako wa hedhi (day one) na siy siku ya kumaliza kuona siku zako (kublidi) kama wengi wanavyodhani.
Kawaida idadi ya siku za siku zako ni kati ya siku 3 mpaka 7. Kila mwanamke ana idadi yake kati ya hizo. Mwingine anaenda siku 3 amemaliza, mwingine siku 4, mwingine 5 mwingine 6 mpaka 7. Chochote zaidi ya siku 7 si cha kawaida na unahitaji kuonana na daktari kwa uchunguzi zaidi.
4. Wingi wa damu
Hii ni Sifa ya mwisho ya mzunguko wa hedhi na inaangalia kiasi cha damu inayotoka wakati wa hedhi. Hapa kuna wanawake wa aina mbili ambapo mwanamke anaweza kutoa damu ya kawaida (normal bleeding) na mwingine akatoa damu nyingi sana (heavy bleeding).
ILI KUZIFAHAMU VIZURI SIKU HATARI KWA MWANAMKE KUPATA MIMBA:
TUANGALIE KIDOGO JINSI MAYAI YANAVYOKOMAA NA KISHA KUTOLEWA KWENYE OVARY.
Fahamu kuwa mzunguko wa ovari (ovarian cycle) ndiyo huleta mabadiliko katika mfuko wa uzazi.
Kwa kawaida mzunguko wa ovari una hatua kuu tatu zifuatazo; Follicular Phase, Ovulation Phase na Luteal Phase.
1. Follicukar Phase
1. Follicukar Phase
Sehemu hii ya mzunguko huanza siku ya kwanza ya mwanamke kuona siku zake mpaka yai linapokuwa limekomaa (graafian follicle)
Mayai ya mwanamke huanza kutengenezwa tangu akiwa tumboni mwa mama yake.
Mpaka kufikia umri wa kuvunja ungo, mwanamke huwa na wastani wa mayai yapatayo 400,000 ndani ya ovari. Mayai haya huwa katika hatua ya uchanga (primary oocyte).
2. Ovulation Phase
2. Ovulation Phase
Katika hatua hii ya mzunguko wa ovari, yai lililokomaa (graafian follicle) hutoka kwenye ovari na kuingia kwenye mirija ya fallopian.
3. Luteal Phase : Hii ni sehemu ya mzunguko wa ovari ambao wenyewe huanza baada ya yai kutoka (ovulation) na kuishia kabla ya kuanza kuona siku zake yaani mwanzo wa mzunguko mwingine.
3. Luteal Phase : Hii ni sehemu ya mzunguko wa ovari ambao wenyewe huanza baada ya yai kutoka (ovulation) na kuishia kabla ya kuanza kuona siku zake yaani mwanzo wa mzunguko mwingine.
Sasa tutaitambuaje siku ya yai kutoka (ovulation)?
Kiuhalisia ni ngumu kujua siku halisi yai lilipotolewa lakini tunaweza kuzitambua siku nyeti ambazo zitatupa nafasi kubwa ya kutokulikosa yai ndani ya siku hizo.
Fuatilia hapo chini.
ZINGATIA HAPA: Idadi ya siku kati ya ovarian cycle na menstrual cycle ni sawa (Mfano, 28, 30, 35, 25).
ZINGATIA HAPA: Idadi ya siku kati ya ovarian cycle na menstrual cycle ni sawa (Mfano, 28, 30, 35, 25).
Idadi ya siku katika luteal phase ni sawa kwa mizunguko yote na ni siku 14.
Folicular phase +luteal phase =Idadi ya siku katika mzunguko[the cycle length).
Lakini tayari tumeshajua luteal phase ni constant,haibadiliki,[ni siku 14 katika kila mzunguko]. ovulation phase hapo iondoe maana ovulation hutokea masaa machache tu.
Sasa ili kuipata siku ya ovulation,tunachukua idadi ya siku katika mzunguko mmoja – idadi ya siku katika luteal phase,ambayo haibadiliki [14 days].
Kwa mfano kwa mwanamke mwenye mzunguko wa siku 28,kuipata siku ya ovulation tunachukua 28-14 tunapata 14, kwahiyo kutoka siku ya kwanza mwanamke alipoanza kubleed ni siku ya 14 ndipo yai linakuwa tayari kurutubishwa.
Kwa mwenye mzunguko wa siku 30, tunachukua 30-14 (luteal phase) =16, kwa hiyo mwanamke mwenye mzunguko wa siku 30, ovulation inauwezekano mkubwa wakutokea siku ya 16 na si ya 14 (kuwa makini hapo).
Yule mwenye mzunguko wa siku 35, ovulation day ni 35-14 = 21, kwa hiyo kwa mwanamke mwenye mzunguko wa siku 35, ovulation ina nafasi kubwa ya kutokea siku ya 21 na si ya 14.
Kwa mwenye mzunguko wa siku 30, tunachukua 30-14 (luteal phase) =16, kwa hiyo mwanamke mwenye mzunguko wa siku 30, ovulation inauwezekano mkubwa wakutokea siku ya 16 na si ya 14 (kuwa makini hapo).
Yule mwenye mzunguko wa siku 35, ovulation day ni 35-14 = 21, kwa hiyo kwa mwanamke mwenye mzunguko wa siku 35, ovulation ina nafasi kubwa ya kutokea siku ya 21 na si ya 14.
Sasa baada ya kuijua siku ya ovulation lazima uwe makini na siku zinazokaribiana na siku ya ovulation kwani nazo ni siku hatari pia.
KWANINI?
Mbegu ya kiume inauwezo wa kuwa hai hadi masaa 48 (2 days) tangu shahawa zimwagwe[ejaculation] na yai lina uwezo wa kuwa hai hadi masaa 24 [one day] tangu lilipotoka kwenye ovary.
Kwaiyo kama mwanaume akijamiiana na mwanamke siku mbili kabla ya yai kutolewa kwenye ovary, mbegu inaweza kuwa hai bado na kutungisha mimba endapo yai litatolewa ndani ya siku mbili zijazo kwa mfano kama siku ya ovulation ya mwanamke ni siku ya 14, mwanamke akijamiiana na mwanaume siku ya 12, uwezekano wa kupata mimba ni mkubwa.
Kadhalika kama mwanamke ametoa yai siku ya 14 kisha akajamiiana ndani ya masaa 24 mbele, pia anaweza kupata mimba kwasababu kipindi mbegu zinamwagwa zinaweza kulikuta yai bado lipo hai na kutungisha mimba.
Kwa ufupi,ni siku tatu tu ndizo hatarishi sana kwa mwanamke kupata mimba,yaani,siku mbili kabla ya ovulation na ndani ya masaa 24 baada ya ovulation[narrow but dangerous window].
Kwa kuongezea,kipindi cha ovulation mwanamke anapata nyege kali sana kwasababu ni kipindi ambacho kuna homoni fulani[androgens] ambazo huchochea nyege huzalishwa kwa wingi. Pia kipindi hicho cha ovulation au karibia ovulation joto la mwili la mwanamke hupanda,anajihisi mwili kuchemka tofauti kidogo na ilivyo kawaida yake.
Sasa, kwa vile nimesema kuwa hatuwezi kuwa na uhakika kwa asilimia 100 wa siku ya kushika mimba, basi tunalazimika kutumia kanuni ya kuepuka tendo la ndoa kwa muda wa wiki nzima. Ambazo ni siku zilizo karibu sana na siku ya kushika mimba (ovulation days) kwa wale wanaotumia njia ya kalenda.
Mfano, kama una mzunguko wa siku 30, kuipata siku ya ovulation chukua 30- 14=16, kwa hiyo siku ya ovulation ni ya 16 tangia ulipoanza kuona damu siku ya kwanza. Sasa kama ni siku ya 16, ondoa siku nne kabla ya hiyo siku ya ovulation.
Kwahiyo kuanzia siku ya 12 hapo, usishiriki tendo la ndoa.
Pia jumlisha siku 3 mbele, ambapo mwanamke atatakiwa kuanza tendo la ndoa kuanzia siku ya 19 huko ili kuepuka mimba.
Ni matumaini yangu umenielewa mpaka hapo
No comments:
Post a Comment