Asikudanganye mtu bwana, uzito mkubwa wa mwili, kitambi na unene vimewanyima wengi sana kuyafurahia mahusiano yao. Najua mara nyingine ni ngumu sana kuwa muwazi kwa mpenzi wako kuhusu uzito wake, unene wake au kitambi chake, na unaona utata kumwambia apungue, lakini hiyo haipunguzi ukweli kwamba haufurahii na unajisikia vibaya, na zaidi ni kwamba unatamani sana apungue. Wala hauhitahi kushurutishwa sana kupungua, faida sio tu kwa mpenzi wako bali kwako pia. Na kama yeye ndicho anachokitamani, inakuwia ngumu nini ku “sacrifice” kwa ajili yake? kwanini kuamua kupungua isiwe zawadi kwake? Najua kuna ugumu, na kuna kujitoa kwa dhati lakini uzuri ni kwamba kujitoa huku kunalipa kwako binafsi na kwa mahusiano yako kwa ujumla.
Monday, 17 September 2018
ZIFAHAMU HASARA ZA KITAMBI NA UNENE KWENYE MAHUSIANO YAKO
Tags
# Mahusiano
# MWANAMKE
About Kichwa's
Kwa matangazo, habari, makala na mambo mbalimbali wasiliana nasi kupitia +255 658 123 572 ama Whatsapp +255 715 665 144.
MWANAUME
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment