ISIKUPITE

Blogroll

Friday, 5 October 2018

BILLNASS AFUNGUKA KUHUSU BIFU LAKE NA DOGO JANJA


Baada ya kutupiana maneno ya kashfa mitandaoni na msanii mwenzake, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ ambayo yalizua gumzo kwamba wawili hao wana bifu kali, mwana-muziki William Lyimo ‘Billnass’ ameibuka na kufunguka.

Awali Dogo Janja aliandika maneno kwenye ukurasa wa Billnass ambayo yalisomeka hivi; ‘Wewe ndiyo maana uliachwa na dada una mdomo sana, hamna mwanamke anaweza kukaa na mwanaume anachamba kuliko mwanamke’, baada ya muda Billnass naye alijibu kwa kuandika; ‘bora kuachwa kuliko kuolewa na mwanamke ili ucheze na mwanaye yeye akienda outings’.

Showbiz lilimtafuta Billnass ili azungumzie ishu hiyo ambapo alisema hana bifu na Dogo Janja bali maneno hayo yalikuwa ni utani tu.

No comments:

Post a Comment