Kutembea ni njia salama na nzuri inayosaidia kuujenga na kuuimarisha moyo uwe na afya nzuri na usio katika hatari ya kushambuliwa na maradhi.
Mazoezi au tabia ya kufanya mazoezi ya kutembea inayo faida kubwa zaidi kuliko matumizi ya dawa.
- Mazoeziya kutembea husaidiakupunguza uzito, tembea dk 60 kila siku
- Ni mazoezi yanayoweza kufanywa na kila mtu
- Ni mazoezi yasiyohitaji vifaa (hayana gharama)
- Ndiyo njia rahisi kabisa ya kuufanya mwili kuwa mkakamavu
- Hupunguza dalili za majonzi na wasiwasi
- Ni mazoezi yenye matokeo ya taratibu
- Hupunguza uwezekano wa kupatwa na kolesto (lehemu)
- Hupunguza na kutibu shinikizo la damu
- Hupunguza uwezekano wa kupatwa na baadhi za kansa
- Hupunguza uwezekano wa kupatwa na kisukari
- Hukufanya ujisikie vizuri
- Husaidia kuimarisha mifupa
- Husaidia kupunguza uwezekano wa kupatwa na shambulio la moyo
- Ni mazoezi uwezayo kuyafanya bila kukusababishia ajari au maumivu makubwa
- Hupunguza mfadhaiko (stress)
- Hupunguza uwezekano wa kupatwa na ugonjwa wa moyo
- Ni mazoezi unayoweza kuyafanya bure bila kulipia chochote
- Husaidia kuimarisha mishipa
- Husaidia katika mfumo wa upumuwaji
- Husaidia kuongeza mzunguko wa damu
Kama afya yako siyo nzuri sana anza kutembea kidogo kidogo labda dakika 10 kwa siku huku ukiongeza dakika 5 kila siku hadi hapo utakapoweza kutembea lisaa limoja mfululizo bila kupumzika.
Ili kupunguza uzito, unene, utipwatipwa, mafuta yaliyozidi au kitambi, fanya zoezi la kutembea kwa miguu mwendo kasi kidogo lisaa limoja kila siku muda wa mwezi mmoja mpaka miwili mfululizo.
Je ni muda gani mzuri wa kufanya mazoezi ya kutembea?,
Wengi wanapenda asubuhi sana na jioni lakini mimi napenda kufanya mazoezi ya kutembea mchana wakati wa jua kali saa sita, saa saba au saa nane, tena huwa natoa kabisa shati na kubaki tumbo wazi.
Utanishangaa kwanini nafanya hivi!, Jua lina umhimu sana kwa afya ya mwili na ngozi pia kama chanzo cha vitamini D, vitamini ambayo ni mhimu sana katika kuimarisha mifupa na hivyo kuzuia ugonjwa wa mifupa (osteoporosis), kuzuia maumivu ya mishipa, kushusha shinikizo la juu la damu, kudhibiti kisukari, kudhibiti kolesto na kadharika.
Unapotembea mchana wa jua kali unaruhusu jua kutua juu yako mwili mzima.
Unajisikia aibu kutembea nje barabarani? au unakosa muda kabisa kwenda kiwanjani kwa ajili ya mazoezi ya kutembea? Kama ni hivyo basi unaweza kununua mashine ya kutembea inayotumia umeme na ukaifunga chumbani kwako na ukawa unajifanyia mazoezi huko huko chumbani kwako, mashine inaitwa ‘TreadMill’. Iangalie kwenye picha hapa chini au namna inavyotumika kwenye video hapo chini zaidi;
No comments:
Post a Comment