Msanii wa muziki Alikiba Alhamisi hii amewatambulishwa wasanii wanne wa label ya King’s Music Label .
Wasanii hao ni 2ga K, Killy, Rasheed pamoja na Abdul Kiba ambaye ni mdogo wa muimbaji huyo.
Muimbaji huyo amewatambulisha wasanii hao ikiwa ni siku moja toka ashambuliwe na mashabiki baada ya kuachia wimbo ‘Hela’ ambao hawakupendezwa nao.
Kiba bado ajaeleza nini kinakuja kutoka kwa wasanii hao licha ya kupost picha za wasanii wao mtandaoni.
Wadau wa mambo wanadai huwenda ni maandalizi ya ujio wa kazi mpya kutoka kwa wasanii hao wapya.
Siku ya jana baada ya kufuta wimbo wake na watu kudai aliufuta baada ya kushambuliwa, muimbaji huyo alifunguka na kudai kwamba alifuta video ya wimbo huo YouTube baada ya kugundua amekosea siku ya kuachia kazi hiyo.
No comments:
Post a Comment